Wednesday, August 16, 2017

Msanii wa Hip hop Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ameshindwa kutimiza ahadi ambayo aliitoa kwa mashabiki wake miezi 7 iliyopita kwamba video yake 'Dume suruali' itakapofikisha jumla ya watazamaji milioni tatu basi angeachia ngoma nyingine.

Inawezekana wazi Mwana FA alitoa ahadi hii akiwa na furaha kwa mafanikio makubwa ambayo video yake ilikuwa imepata ndani ya muda mfupi kwani ndiyo video yake ya kwanza kuweza kuwa na mafanikio ya juu kwenye mitandao ya kijamii hususani You Tube.
Novemba 25, 2016 Mwana FA aliachia video ya 'Dume Suruali' na ilipofika Januari 11, 2017 ilikuwa imefikisha jumlaa ya watazamaji milioni moja kitu ambacho kwa Mwana FA kilikuwa ni kikubwa na yeye alikiri kuwa si jambo la kawaida kwake. 
"Najua kwa baadhi ya wasanii hii siyo namba kubwa hata,ila kwangu 'its a big deal' sababu haijawahi kufika kamwe! nawashukuru sana, salutes nyingi, heshima kwenu, ninyoosheni kwa kuifikisha angalau milioni mbili ama tatu nizidi kuwakubali tafadhali endeleeni kuangalia mnikomoe" aliandika Mwana FA kupitia Instgram yake 
Na kweli mashabiki wa Mwana FA waliendelea kumkomoa kwa kumuingizia mkwanja bila kuchoka kwa kutazama video hiyo ambayo hata Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Pombe Magufuli bila shaka alikuwa akiitazama kutokana na kuvutiwa na utunzi na ufundi wa mashairi jambo ambalo Rais alishindwa kuvumilia mpaka kumpigia simu Mwana FA na kumpongeza kwa wimbo huo. 
Tarehe 16 Januari video hiyo ilifikisha watazamaji milioni mbili jambo ambalo lilimfanya Mwana FA kuwa na furaha zaidi na hapo ndipo alipotoa ahadi akiwa na furaha na kusema labda ngoma hiyo ikifikisha watazamaji milioni tatu angeweza kuachia ngoma nyingine. 
"Najua kwamba siyo namba kubwa hii kwa baadhi ya wasanii, 'actually' ni kanamba flani kaduchu tu,ila kwangu 'its a big deal' kwa hivyo sitakaa niigize hapa kuwa 'this is how we do it' na 'it's normal', no it's not, siyo kawaida..Nashangaa, ahsanteni sana. 'how about tukifika 3 milioni tunatoa ngoma nyingine? now lets get to 3 milioni" alisisitiza Mwana FA kupitia ukurasa wake wa Instgram 
Kutokana na uzuri wa ngoma hiyo watu waliendelea kumnyoosha Mwana FA kwa kuzidi kuitizama video hiyo, ikafikisha watazamaji milioni tatu lakini jamaa akapiga kimya, mashabiki wakaendelea kufuatilia ngoma hiyo mpaka sasa ambapo tayari umefikisha watazamaji zaidi ya milioni nne, yaani naweza kusema video hii imekwenda mbele ya matarajio ya Mwana FA kwani mwanzo alionekana kuwa na mashaka huenda isiwe na mafanikio hayo lakini kila alipoweka lengo ifike kiasi fulani ilifika na kuvuka.
Wimbo wa 'Dume Suruali' Mwana FA alishirikiana na Vanessa Mdee, ulitengenezwa na mtayarishaji Daxo Chali kutoka Mj Records na video yake ilitengenezwa nchini Afrika Kusini na Studio Space Pictures. 

0 comments:

Post a Comment