Monday, August 21, 2017


NAIROBI, KENYA: Rais Mteule, Uhuru Kenyatta ameruhusu maandamano ya amani ya kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.


Kenyatta amewataka Polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi watu wakati wa maandamano hayo.
Rais huyo Mteule alisema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumanne iliyopita. Kenyatta alisema hayo akiwa Jengo la Harambee alikokwenda kukutana na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya kuapishwa kwake.

0 comments:

Post a Comment