Posted by Williammalecela.com on Monday, August 21, 2017
 |
Watendaji wachache wa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wametia dosari jina Halmashauri kwa Uzembe na Kutokujua sheria. Kwamba Leo wameamka na Kuongeza Ushuru kutoka kiasi cha shillingi 500 mpaka 1000,bila kujua kuwa Sheria hairuhusu jambo Hilo.
Tumeagiza kurudi kiasi kilekile cha shillingi 500 kwa siku kwa kila
daladala,kwakuwa Baraza la Madiwani halikuongeza kiasi hicho kama
inavyotakiwa na Sheria, na Baadae Mabadiliko hayo kusainiwa na Waziri Mwenye Dhamana na TAMISEMI, ndiyo ianze kutumika. Lakini hakuna Maombi ya Namna hiyo taliyotolewa na Baraza la Madiwani na Hakuna Waziri aliyeruhusu jambo hilo.
Kama Meya wa Halmashauri ya Manispaa ubungo,nimesikitishwa na Watendaji
wetu wa Halamshauri kutuingiza kwenye Mgogoro na Watumiaji wa Hiduma
hii bila sababu za Msingi,Tunasubiria vikao tuh kuchukua hatua kali za
Kinidhamu kwa mujibu wa kisheria. Aidha kuhusu Baraara ya simu
2000 kuwa Mbovu,nimeelezea kuwa hiyo barabara pesa zake zimezuiwa kwa
sababu za kisiasa,Lakini pesa hizo zipo tangu 2015, kiasi cha shillingi
Billioni 1.7 kutoka BENKI YA DUNIA,pamoja na Wizara ya fedha kuzuia
fedha za fidia ndicho kinacho chelewesha barabara kuendelea kuwa Mbovu MWISHO
Hatua kali za kinidhamu kwa waliopandisha Ushuru kinyume na Sheria
inavyotaka;kwa Madiwani kukaa na kupanga na kisha waziri kupitisha
zitachukuliwa kwa waliohusika,na Kero ndogondogo za stendi kama walinzi
na wahudumu wa vyoo pia zita shughulikiwa HARAKA SANA. Boniface Jacob Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Senior councilor Ubungo. |
0 comments:
Post a Comment