Monday, August 21, 2017

Image may contain: one or more people and text

Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro.

Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi. “Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja.
Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.
“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi.
Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.

0 comments:

Post a Comment