Thursday, August 31, 2017



Lemutuz.com kuanzia hivi sasa itakuwa ni sehemu sahihi zaidi kwako kupata taarifa mbalimbali za michezo kutoka katika kila pande ya dunia kwa muda na wakati sahihi. Utapata tetesi zote za usajili barani Ulaya na Kuangalia michezo mbalimbali mubarashara 'LIVESTREAMING' katika simu, tablet au Computer yako.

Ungana na Lemutuz.com hapa chini kupata tetesi mbalimbali za usajili barani ulaya siku ya leo:-
 

Klabu ya Everton wamepanga kufunga dirisha la usajili kwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Fc, Michy Batshuayi ili kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji huku mkufunzi wa timu hiyo Ronald Koeman anaona usajili wa nyota huyo akiungana na Wayne Rooney utaleta chachu katika timu hiyo.(Chanzo: Daily Express)

Klabu ya Arsenal watamuuza Alexis Sanchez kwenda Manchester City endapo watafanikiwa kuinasa ya saini ya mshambuliaji hatari wa PSG, Mjerumani Julian Draxler. Wakati huo tayari klabu ya Arsenal imemruhusu kiungo Alex Oxlaid-Chamberlain kwenda Liverpool FC kwa Paundi milion 35. (Chanzo: Daily Mirror)

 
Hapo awali AS Monaco walikataa kumuuza mchezaji wao Thomas Lamar kwenda Liverpool Fc, lakini hivi sasa mambo yanaonekana kubadilika baada ya kukubali kumuuza iwapo klbau ya Liverpool Fc itakuwa tayari kulipa kitita cha €100m kwa nyota huyo. (Chanzo: )


 
 Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza Chelsea Fc, wako katika mazungumzo mazito na klabu ya Swansea City ili kumsajili mshambuliaji wao, Mhispaniola Fernando Llorente. Dili hili linatarajiwa kufanyika ili kuongeza nguvu katika safu ya uhsambuliaji katika timu hiyo baada ya Diego Costa kugoma kurejea Uingereza huku akilazimishwa kuuzwa Atletico Madrid. (Chanzo: Sky Sports)

 
Klabu ya Borrusia Dortmund imefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji Jeremy Toljan kutoka klabu ya TSG Hoffenheim kwa ada ambayo haijawekwa wazi. (Chanzo: Goal.com)

Image result for jurgen klopp on transfer images
Jurgen Klopp amepanga kutumia kiasi cha £175m leo hii katika dakika za lala salama za dirisha la usajili katika majira ya joto kwa kuwasajili Alex Oxlade-Chamberlain, Thomas Lemar na Virgil van Dijk ili kuongeza nguvu katika kikosi chake. (Chanzo: The Times)

 Image result for diego costa to atletico madrid
Diego Costa anatarajiwa kukamilisho uhamisho wa £50m kutoka Chelsea Fc kwenda Atletico Madrid, lakini hatoweza kujiunga na timu hiyo mpaka hapo Januari katika dirisha dirisha la usajili majira ya baridi. (Chanzo: Agent Mike)


Mshambuliaji wa Ureno, Luis Nani amewasili Jijini Rome huko Italy tayari kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Valencia kujiunga na S.S Lazio. (Chanzo: Calciomercato)

Endelea kutembelea www.lemutuz.com kwa taarifa mbalimbali za michezo hususan tetesi za usajili barani ulaya na kutazama michezo mbalimbali 'MUBASHARA' ikiwemo Ligi Kuu zote barani Ulaya na Michuano ya Ligi Mabingwa barani Ulaya


Categories:

0 comments:

Post a Comment