
Mshambuliaji wa Hipsania mwenye asili ya Brazil, Diego Costa anayekipiga katika klabu ya Chelsa amejumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea msimu huu licha ya mtafaruku uliopo kati yake na timu hiyo.
Chelsea inaonekana imekubali ayishe na wamemaliza tofauti zao baada ya Mhispania huyo kutajwa katika kikosi
cha timu hiyo kinachoshiriki Ligi Kuu England msimu huu.
Mhispania
huyo aliweka mgomo na kulazimisha kutaka kurejea Atletico Madrid baada
ya bosi wa Blues, Antonio Conte kumtumia ujumbe wa kumtaka aondoke.
Mbali
ya Chelsea, pia Liverpool na Arsenal zimefanikiwa kushinda vita zao na
wachezaji wao wanaotaka kuondoka Philippe Coutinho na Alexis Sanchez
wametajwa katika orodha ya wachezaji 25 watakaowatumia katika msimu.
Coutinho
alikuwa akihusishwa kutakiwa na Barcelona kwa muda mrefu, wakati
dirisha la usajiki Hispania likifungwa leo usiku bado kuna uwezekano wa
kujiunga na miamba hiyo Catalans.
Huku Alexis Sanchez alikuwa
na hamu kubwa ya kuondoka Arsenal kujiunga na Manchester City, lakini
Gunners ilikataa dau la City la pauni 60milioni.
Costa, 28, yuko nyumbani kwao Lagarto, Brazil na kukosekana kwake mazoezini kwa siku 14 atakuwa akitozwa faini ya pauni 300,000.
Chelsea
na Atletico sasa wanaweza kujadiliana kuhusu kumruhusu mshambuliaji
huyo kurejea Madrid, japokuwa kikwazo kikubwa ni ada ya uhamisho.
Chelsea inataka walipwe pauni 50milioni kwa mshambuliaji huyo waliyemnunua kwa pauni 32milioni miaka tatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment