Tuesday, September 5, 2017

Kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania wakishirikiana na Finca leo wamezindua huduma ya Benki ya mkononi (HALO YAKO) ambayo itasaidia huduma za kifedha haswa kwa maeneo ya Vijijini.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mr. Le Van Dai ambaye ni Mkurugeni Mtendaji  wa Halotel Tanzania amesema huduma hiyo itaweza kukuza uchumi na itaweza kuboresha maisha ya watanzania.

"Tunashukuru sana uhusiano ambao tumeujenga kati yetu na Finca ambapo miaka mingi wamekuwa wakitoa huduma za kifedha kwa jamii ya watanzania " alisema Le.

Amesema watu wa vivijini walikuwa na shida ya kufikiwa na huduma ya kifedha kwa njia ya simu na maendeleo ya kitekinolojia yametoa fursa kwa Kampuni ya mawasiliano ya simu ya halotel na kushirikiana na Finca Microfinance Bank. 

Aidha huduma ya HALO YAKO inapatika kupitia huduma ya HALOPESA inayotolewa na kampuni ya Halotel ambayo ni huduma ya kifedha inayomwezesha mteja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi  na kwa usalama.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Finca Issa Ngwengwe amesema wameungana na Halotel kufanikisha huduma hiyo kwa watumiaji na wataweza kuwa na akaunti ya Bank kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo ambaye amekuja kwa niaba ya Waziri wa fedha ambaye ni kamishna wa fedha za nje John Lubuga amesema serikali iko tayari kushirikiana na kampuni mbalimbali zenye malengo ya kuondoa umasikini kwa watanzania hivyo wanaipongeza Halotel na Finca.















0 comments:

Post a Comment