Monday, September 4, 2017

Msanii Sajna amekanusha taarifa za yeye kutumia madawa ya kulevya, na kusema kuwa taarifa hizo zinazushwa na watu na hazina ukweli wowote, kwani hajawahi hata kuyaona madawa hayo.

 Sajna amesema hajawahi kuyaona madawa hayo kwa macho hata kuyashika, zaidi ya kuyasikia tu.
"Yale maneno maneno ya mtaani sijui Sajna anatumia nini sio kweli ni maneno tu, mi hata kuuona sijawahi kuona kwa macho", alisema Sajna.
Sajna ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na nyimbo yake mpya ya 'uko wapi', amesema mabadaliko aliyo nayo ya muonekano wake yametokana na kukua, na sio matumizi ya madawa ya kulevya.

0 comments:

Post a Comment