![]() |
| Baraka Joshua maarufu kama (Mtoto wa Nyani ) akiingia kwenye Gari ya Polisi kuelekea gerezani |
Kijana aliyeishi na nyani tangu alipozaliwa hadi kufikia umri wa miaka 9 baada ya kutupwa msituni na Mama yake Mzazi mkoani Shinyanga amehukumiwa kwenda jela maisha na miaka mingine 30.
Hukumu hiyo imetolewa leo Mahakama ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo Kijana huyo anae fahamika kwa jina la Baraka Joshua Maarufu Kama (Mtoto wa nyani) ambae alikuwa nje kwa dhama.
Akisoma Hukumu hiyo leo, Hakimu Catherine Kiyoja amesema Mahakama imeridhika na ushahidi uliuotolewa Mahakamani hapo ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa.
Hakimu alisema katika ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na shahidi namba moja ambaye ni malalamikaji alisema siku ya tukio Mshtakiwa huyo alimkamata na kisha kumuingilia kwa nguvu sehemu zote mbili ambapo alimbaka nakumlawiti.
Kwa upande wa Daktari wa Hospital ya Amana amesema alimpokea mtoto huyo aliefanyiwa tukio hilo na kumfanyia vipimo ambapo aligundua kuwa likuwa amebakwa.
Hakimu alimwambia mshtakiwa kama ana chochote cha kuiambia Mahakama na kujitetea kabla ya kupewa adhabu, mshtakiwa huyo alijibu hana chochote cha kuongea.
Hakimu alimuuliza mwendesha mashtaka SP Munde Kalombola kama kuna kumbukumbu za nyuma za makosa ya mshtakiwa, ambapo alijibu hakuna ila apewe adhabu kutokana na kosa alilofanya.
Hakimu amemuhukumu kutumikia kifungo cha maisha kwa kosa la ulawiti na kosa la pili la ubakaji kifungo cha miaka 30.

0 comments:
Post a Comment