Wednesday, September 6, 2017



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa na Madaktari Wanajeshi


Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika upimaji afya bure kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.


Zoezi hilo ambalo kwa leo limesimamiwa vizuri na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Mokonda na kuweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa namba pamoja na kuendesha zoezi hilo vizuri.

Moja kati ya watu waliofika katika eneo hilo Rehema Mussa alisema anashukuru sana  kwa zoezi hilo kwani wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali lakini uwezo wa kifedha hauko vizuri hivyo wanashindwa kufanya vipimo.

"Mimi nasumbuliwa na mgongo na kiuno kwa muda mrefu leo nimefika hapa tangu asubuhi nangoja foleni yangu ifike niweze kupatiwa vipimo" amesema Rehema

Mkazi mwingine wa Dar es Salaam Juma Hassan amesema amefurahishwa na Mkuu wa Mkoa kwa kusema wataletewa Mahema kwa ajili ya kivuli na pia watapewa maji ya kunywa kwa siku ya leo.
Mkuu wa mkoa akizungumza na waandishi wa habari




0 comments:

Post a Comment