Mjumbe wa NEC, na mjumbe wa kamati kuu (CCM) ambaye pia ni meya wa Manispaa ya ilala jijini Dar es Salaam anayemaliza muda wake Mhe.Jerry William Silaa akiwasili kituoni kwa kupiga kura mapema leo akiongozana na mkewe na mtoto wao wa kwanza katika kituo chake cha kupigia kura eneo la Guluka Kwalala leo ikiwa ni hatua muhimu kufuatia zoezi linaloendelea leo la chaguzi za ndani za ccm nchi nzima kwa makada wa Chama Cha mapinduzi kwa ajili ya kura za maoni.
Mhe Jerry Silaa anapiga kura pia akiwa kama mmoja wa wanachama wa chama Cha mapinduzi wanaoomba kuteuliwa na chama Chake katika jimbo la ukonga kupeperusha Bendera ya Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika tarehe 25/10/2015 nchi nzima.
Ikumbukwe Mhe.Jerry Silaa ameshawaletea maendeleo mengi kwa muda mfupi aliokaa katika nafasi ya udiwani wa kata ya Gongolamboto na Manispaa ya Ilala ikiwa ni pamoja na kuwapatia wananchi maendeleo mbalimbali ikiwemo miundo mbinu ya barabara,upimaji viwanja,Elimu,kiuchumi na mengine mingi ambapo mengi ya mambo hayo yalikuwa katika ahadi zake na ilani ya chama cha mapinduzi .
''......Kiukweli tunamshukuru sana Mhe.RidhiwaniJerry Silaa kwa kukubali kuja kuomba ridhaa ya kutuongoza kwani ametusaidia wana ccm wa kata zote za ukonga wamuunge mkono Mhe.Jerry ili atuwakilishe Dodoma 2015.....Aliskika mkazi mmoja akisema baada ya kufanya mahojiano na blogu hii..''
Masama blog ilitaka kujua ni kwa nini Mhe.Jerry Silaa amechukua form ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa jimbo la ukonga kwa miaka mitano ijayo?
''....Kwanza ninapiga kura ikiwa ni moja ya haki yangu katiba na kutekeleza sera ya chama chetu na pia yakiwa ni maombi yangu ya dhati kwa wana ccm wenzangu na jimbo la ukonga wanipe nafasi ya kuwa mgombea wao ili niende kundeleza kazi ya kusimamia ilani kwa hatua kubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa ukonga na watanzania kwa ujumla......''
Masama Blog tunaungana na wana cukonga wote kukutakia Kila la Heri na Afya njema katika kufikia hili lengo la ushindi na hatimaye kuwawakilisha wananchi wa Chalinze katika bunge la 11 la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani tunaamini uwezo na weledi wako katika kuwatumikia wananchi.




0 comments:
Post a Comment