Baada
ya kutoa wimbo mpya, Nyumbani Kwetu, Nay wa Mitego amedai kuwa amepokea
changamoto za baadhi ya wasanii kumdiss kuwa amehama kwenye hip hop na
kufanya muziki mwingine.
Nay ameiambia Bongo5 kuwa anafanya muziki unaohitajika na mashabiki wake na yupo tayari kuimba hata Taarab kama itamlipa.
“Wapo ambao wanaendelea kudiss nimetoka kabisa kwenye Hip Hop na
sipaswi kujiita mwanahiphop. Muziki ndio kazi yangu na ninafanya kile
wanachohitaji mashabiki, nitaimba hata Taarab kama itakuwa inalipa,”
amesema Nay.
“Mimi hata wakidiss, kwangu ni furaha tu. Mimi ninachoangalia ni
hela. Ni mwanamuziki mfanyabiashara, muziki ninaoupenda ni hip hop na
ninaufanya hata kuliko wanavyofanya wao. Nikifanya huu pia nafanya
kuliko hata hao wanaofanya. Mimi naangalia mashabiki wangu wanataka
nini. Wanadiss wakati wanasikiliza nyimbo zangu ndio maana wanapata
nafasi ya kudiss.”
0 comments:
Post a Comment