Monday, November 9, 2015

WATEULE CHADEMA VITI MAALUM MBEYA NI SONGOMBINGO TUPU!!!!
WALIOSTAHILI WADAIWA KUPIGWA CHINI.



“Hapa simung’unyi maneno kabisa. Kwa mfano aliyeteuliwa mkoani Ruvuma, hata viongozimkoa huo hawamjui. Kutoka Iringa wameteuliwa watatu, lakini mmoja amejiunga Chadema hivi karibuni na jina lake linateuliwa. Hapa Mbeya ameteuliwa mmoja, lakini ushiriki wake kwenye chama unazidiwa na wanawake wengine walioomba nafasi hiyo waliopo hapa na huko mkoani Songwe ambako kuna majimbo matatu ya Chadema hajateuliwa mwanamke hata mmoja, Je hii ni halali?, alihoji Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya wagombea Ubunge kupitia Chadema na Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bwana Jacob Kalua.
Naye Katibu wa Chadema, Wilaya ya Mbarali Nicolaus Lyaumi alisema anashangazwa kuona majina ya wabunge walioteuliwa siyo wale waliotarajiwa na wanachama wengi mkoani Mbeya.
“Unajua lengo la wabunge hawa ni kusaidia ujenzi wa chama mkoa na wilaya husika , lakini sasa kwa uteuzi huu tunaamini kabisa bado kuna sintofahamu iliyo mbele yetu kwani watu waliomba wamepigwa chini,”.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la ‘China’ alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia chochote akisema hajapata orodha kutoka kwa viongozi wake na kwamba majina yaliyotangazwa hayaamini.
(C) Mwananchi E-Paper 8/11/2015.


Kwa Mtindo huu, Demokrasia itapiga hatua katika Upinzani hapa Nchini???

0 comments:

Post a Comment