Thursday, December 10, 2015


    NIMESTAAFU


    Mwaka 2010,nilipata heshima ya kuaminiwa na Madiwani wenzangu pamoja na wananchi kuwa Meya wa Kinondoni.Mwaka 2015, kwa hiari yangu niliamua Kustaafu na hivyo sitakuwa tena Meya wa Kinondoni.
     

    Nashukuru kwa heshima hii na kwa pamoja tumeifikisha Kndoni hapa ilipofika. Najua bado kuna changamoto lakini tumepiga hatua kubwa sana na kuifanya Kndoni kuwa Manispaa bora TANZANIA ktk maeneo mengi.
     

    Tumeboresha sana Mapato toka 10 bln mpaka 50 bln zitakazokusanywa mwaka 2015/16; tumeweka nidhamu kubwa ya matumizi, zaidi ya 60% ya Mapato ya ndani yanatumika ktk miradi ya maendeleo; tumeboresha sana huduma za jamii- Elimu na Afya; ktk kupunguza msongamano tumejenga madaraja na barabara; tumejenga Masoko ya wafanyabiashara; Tumetoa na kutenga Mikopo kwa Vijana na wanawake zaidi ya 2bln; tumejenga Umoja, kuboresha michezo pamoja na kuwa na timu ya mpira wa miguu inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
    Ktk kipindi hiki Kndoni imebadilika na kuwatofauti sana.



    Kndoni sasa inajulikana kwa mazuri TANZANIA na AFRIKA. Tumedhihirisha hayo kwa kupata tuzo na pesa TANZANIA NA AFRIKA.Naamini tutapata viongozi wazuri watakao yaendeleza mazuri na kuipeleka mbele zaidi Kndoni
    Nawashukuru sana Wanakinondoni, Naibu Meya Songoro,Wah. Madiwani wote, Mkurugenzi Natty na Wafanyakazi wote wa Kndoni kwa kushirikiana pamoja bila kujali tofauti za itikadi na kuifikisha Kndoni ilipofika . Nimestaafu uongozi wa kuchaguliwa lakini bado kama mwana Kndoni nitaendelea kusaidia utatuzi wa changamoto za Kinondoni kwa kadri nitakavyoweza
    .


    NAWATAKIA KILA LA HERI VIONGOZI WA KIPINDI HIKI CHA HAPA KAZI TU.
    MUNGU IBARIKI KINONDONI

0 comments:

Post a Comment