STAA wa filamu Bongo, Aunt
Ezekiel amesema hakuna kitu ambacho anajivunia maishani kama kupewa
penzi motomoto na mpenzi wake, Moze Iyobo.
Akipiga stori hivi karibuni na paparazi
wetu, Aunt Ezekiel aliweka wazi kwa kusema kwamba anajivunia kuwa na
Iyobo kwani ni mwanaume sahihi kwake na amekuwa akimfanya kuwa na furaha
muda wote.
“Najisikia raha sana kuwa na Iyobo wangu
na ndiyo maana utaona kila sehemu nafuatana naye, hana makuu ingawa
katika maisha kukwaruzana kupo ila yeye ni mstahimilivu kupita maelezo,
naweza kusema tangu niyajue maisha ya mapenzi, Moze ni mwanaume ambaye
nimeishi naye kwa amani na upendo hivyo naomba Mungu aendelee kunijalia
zaidi tutimize ndoto zetu,” alisema Aunt Ezekiel.

0 comments:
Post a Comment