Wednesday, December 9, 2015

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Johnson Minja amesema Tanzania imepata rais ambae anafanana na watu wake, kwani viongozi wote wakubwa akiwemo makamu wa rais na waziri mkuuu wameungana na watanzania wote kushiriki zoezi zima la usafi, ili kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

 Pia Minja amesema kuwa suala la usafi liwe endelevu kwa watu wote bila kujali itikadi na kumtaka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie, ili mazingira yawe safi na salama kwa afya ya kila mtanzania na kuongeza kuwa suala la usafi kwa vitendo linaipa sifa Taifa kwa wageni mbalimbali wanaokuja kwa ziara za matembezi nchini

0 comments:

Post a Comment