Sunday, December 20, 2015

gereji
 

Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, limeeleza nia yake ya kutafuta namna ya kuwabana wanaoendesha shughuli za kuchomelea vyuma kwenye makazi ya watu ambayo hayajawekewa nguvu kubwa ya umeme ya kuwezesha kuendesha mashine zao.

Kwa mujibu wa Tanesco, biashara hiyo kwa sasa imezidi kushamiri kwenye maeneo mengi nchini na wanaoendesha biashara hiyo wamekuwa hawaombi vibali Tanesco kwa ajili ya kuunganishiwa umeme unaoendana na nguvu ya mashine zao.

Akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina ya wenyeviti, watendaji na wajumbe wa serikali za mitaa wilaya ya mbagala mkoa wa Tanesco wa Temeka jijini Dar es salaaam, Mkuu wa Idara ya Mipango Tanesco mkoa wa Temeke, Injinia Ffrank Chambua amesema watu hao wanasababisha kuwepo na tatizo la upungufu wa umeme kwenye mkoa huo na kuwataka watendaji hao kushirikiana na Tanesco kuwabaini ili wachukuliwe hatua.

Baadhi ya wenyeviti, watendaji na wajumbe wa serikali za mitaa wilaya ya mbagala waliohudhuria mkutano huo, wakizungumza na channel ten wameitaka Tanesco kuwa na utamaduni wa kushughulikia matatizo au malalamiko yanayowasilishwa kwao kwa haraka .

Mkoa wa Tanesco Temeke una jumla ya wateja halali elfu sitini waliounganishiwa umeme na Tanesco

0 comments:

Post a Comment