Friday, January 22, 2016




HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imeboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa nje ili wapate muda zaidi wa kutibiwa na kupata ushauri wa daktari katika kliniki mbalimbali.

Uboreshaji huo utasaidia wagonjwa kupata huduma kwa wakati na kupunguza muda wa kusubiri kupata huduma hata msongamano katika eneo moja ndani ya hospitali.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa Nje, Dk Raymond Mwenesano wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema utaratibu huo utawasaidia wagonjwa wanaokwenda kutibiwa na kuondoka hususan wale wanaolipia fedha taslimu, wagonjwa ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), bima mbalimbali za afya pamoja na watumishi ambao kampuni zao zina mikataba na hospitali kutibu wafanyakazi wao.

0 comments:

Post a Comment