Chama
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Rukwa, kimewataka vijana
wote ambao ni wanachama na washabiki wa chama hicho mkoani humo,
watambue kuwa kipindi cha uchaguzi kimeshapita na wala sio wakati wa
kutamani kufanya kampeni na maandamano,hali inayochangia kuwepo kwa
migogoro ya mara kwa mara ndani ya chama, bali sasa waelekeze maisha yao
katika kufanya kazi na uzalishaji.
Mwenyekiti wa chama cha chadema mkoani Rukwa Bw.Zeno Nkoswe,
akiongea mjini Sumbawanga amesema wamebaini kuwa migogoro mingi na
isiyoisha inayoendelea ndani ya chama hicho hivi sasa,ni vijana
kutojitambua kuwa sasa kampeni zimeisha na uchaguzi umepita na kwamba
kuna maisha baada ya uchaguzi,na wengi wanaojihusisha na migogoro hiyo
ni wale walioshiriki kwenye kura za maoni,na pia ameeleza kuwa tofauti
zao na makao makuu ya chama zilimalizwa na mratibu wa chama hicho kanda
ya nyanda za juu Bw.Frank Mwaisumbe.
Kwa upande wake katibu wa chadema wa wilaya ya Sumbawanga mjini
Bw.Pius Nguvumali,amesema anashangazwa na kitendo cha waliokuwa wagombea
ubunge katika majimbo ya kwela na nkasi kusini kupitia chama hicho,
ambao sasa wamehamishia shughuli zao mjini hapa na kuchochea migogoro,
wakati chama kikifanya tathmini ya ushiriki wao kwenye uchaguzi mkuu
kujua walikosea wapi na kujipanga kwa upya.
0 comments:
Post a Comment