SHERIA za Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka
2015, imesaidia kupunguza makosa ya mtandao kwa asilimia 60 tangu kuanza
kutumika Septemba mosi, mwaka jana.
Hatua hiyo imetokana na wananchi kuanza kuelewa matumizi bora ya
mitandao na kuwezesha matumizi ya mtandao kutumika kwa jinsi
ilivyokusudiwa .
Hayo yalisemwa jana katika kikao cha kujadili sheria hiyo kwa
wafanyakazi na walimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
kilichofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Kitendo cha Sheria katika
wizara hiyo Kitengo cha Mawasiliano, Veronika Sudayi alisema kati ya
makosa yaliyokuwa yameshamiri na sasa kupungua kwa kiasi kikubwa baada
ya kuanza kutumika sheria hiyo ni picha za ngono mitandaoni, makosa ya
udhalilishaji watoto na watu wazima.
Sudayi alisema kuna makosa ambayo bado yanaendelea kwa kasi
mitandaoni yanayohitaji kuchukuliwa hatua stahili ikiwemo elimu kwa umma
ambayo ni uchochezi na taarifa za uongo unaofanywa na kundi kubwa la
vijana.

0 comments:
Post a Comment