Posted by Williammalecela.com on Tuesday, January 26, 2016
Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20,
mwaka huu, umesababisha Chama cha wananchi (CUF) kushindwa kufanya
maadhimisho ya kuwakumbuka wenzao waliofariki dunia mwaka 2001.
Maadhimisho hayo hufanyika Januari 27 ya kila mwaka yakishirikisha viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na wafuasi wake.
Akizungumza jana, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama
hicho Taifa, Abdul Kambaya, alisema uongozi wa CUF taifa hautafanya
maadhimisho hayo kwa kuwa siku hiyo Kamati Ttendaji itakuwa inafanya
kikao cha kujadili tarehe ya marudio ya uchaguzi ambayo ilitangazwa hivi
karibuni na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).
Kambaya alisema siku hiyo kamati itakutana kuandaa ajenda kuhusiana
na kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi ambazo zitapelekwa katika
Baraza Kuu la chama.
“Ni vijana tu ndiyo watafanya maadhimisho hayo kwa upande wa
Zanzibar na ndiyo ambao watafanya maandamano ya kukumbuka mauaji hayo.”
Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kama kumbukumbu ya
kuomboleza vifo vya wafuasi wa chama hicho waliouawa Januari 27, mwaka
2001 wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais visiwani humo.
0 comments:
Post a Comment