MAMIA ya wakazi wa Wilaya ya Kinondoni wamejitokeza kupima afya zao
ikiwemo ugonjwa wa moyo, katika kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Paul Makonda kwa lengo la kuhamasisha wakazi wa wilaya
hiyo kupima afya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mganga
Mkuu wa Wilaya hiyo, Aziz Msuya alisema kuwa wananchi wameitikia mwito
huo na wanatarajia kuendelea leo.
Alisema kuwa wingi wa watu waliojitokeza katika kampeni hiyo viwanja vya Leaders, umesababisha kupungukiwa kwa vifaa.
“Mpaka sasa wananchi 2,000 wamepimwa na wengine wanasubiri huduma.
Vifaa tulivyokuja navyo vimekuwa pungufu kwa sababu ya wingi wa watu,”
alisema Msuya.
Aliongeza kuwa magonjwa yanayopimwa ni kisukari, presha na moyo
ambapo baadae wanatakiwa kwenda katika Hospitali ya Mwananyamala au
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Pia alitoa wito kwa wakazi hao kutowatoa wagonjwa wao ambao wako
hospitali kwani kitendo kinachofanyika katika kampeni hiyo ni kupima na
sio kutibu.
0 comments:
Post a Comment