Monday, January 25, 2016

Obama: Siwezi kugombea Urais tena.


Rais wa Marekani Barack Obama, amesema hata kama ingepitishwa hawezi kugombea muhula wa 3.

Akizungumza na kituo cha CBS asubuhi ya leo, Obama amedai yeye ni binadamu, kukaa madarakani kwa muda mrefu kunaweza kuivuruga akili yake.

Amesema mkewe anahitaji sana kuwa nae karibu, hivyo Michelle angekuwa wa kwanza kupinga swala la kugombea tena.

“Ile ni ofisi inahitaji kupokezana, mawazo, msimamo na ubunifu mpya kila siku, ingefika kipindi nisingeweza kwa sababu akili itakuwa imechoka” alisema.

0 comments:

Post a Comment