Thursday, January 28, 2016




KIWANGO cha Kodi ya Mshahara (PAYEE) kinatarajiwa kushushwa hadi asilimia 10 katika mwaka ujao wa fedha wakati serikali ikiendelea kujadiliana na vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kuipunguza hadi kufikia tarakimu moja.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema pia wanaangalia uwezekano wa kupunguza kiwango kikubwa cha kodi kwa watumishi waandamizi ambao wamekuwa wakilipa asilimia kubwa kutokana na mishahara yao mikubwa.

Alisema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Chakoma (CCM) aliyetaka kufahamu serikali imejipangaje kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015 inayolenga kuwapunguzia wafanyakazi PAYE kutoka asilimia 11 hadi tarakimu moja.

“Baada ya kufikia kiwango hicho cha asilimia 10, serikali itaendelea kujadiliana na vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kupunguza PAYE hadi kufikia tarakimu moja kutegemea na hali ya uchumi utakavyokuwa unaimarika mwaka hadi mwaka,” alisema.

Kima cha chini kisichotozwa kodi ni kipato cha mshahara kisichozidi Sh 170,000. Alifafanua kuwa watumishi waandamizi wanalipa kodi kubwa kutokana na mishahara yao mikubwa na kwa asilimia kubwa zaidi ya wale wa chini

0 comments:

Post a Comment