Thursday, February 11, 2016

Mawaziri Wawili wa zamani wa Serikali ya Rais Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Fedha kulia Mramba na aliyekua Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona, baada ya kutumikia kifungo cha Mwaka mzima Jela majuzi waliachiwa na kuanza kutumikia kifungo cha nje ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa Mazingira Hospitali ya Palestine, hapa wakipewa darasa na msimamizi wao namna ya kufanya usafi baada ya kuvalishwa uniform maalum. Hii ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa Mawaziri wa zamani kudhalilishwa mbele ya hadhara kwa kmakosa waliyoyafanya wakiwa madarakani, kulia ni aliyekuwa Waziri wa Fedha Mramba ambaye wakati mmoja aliwahi kusema "Hata kama ikibidi wananchi watakula majani lakini lazima Rada inunuliwe na Serikali".

1 comment:

  1. Mwizi ni mwizi tu. Sio waiba kuku pekee yao ndio wezi, tena hawa ni majambazi yaliyowaweka watu katika hali ngumu. Kwanza hii azabu ni ndogo sana. Kwao. Nchi zilizoendela adhabu wangetumikia tena kwa muda mrefu. Walivyoiba vingerudishwa wangefirisiwa. Na kama ingekuwa nchi za asia adhabu yake ni kunyongwa

    ReplyDelete