Saturday, March 19, 2016


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.


Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam na mbunge wa jimbo la Ukonga Mhe. Waitara Mwita amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa sheria inaruhusu kikao hicho kuhudhuriwa na wananchi wote hivyo kwa kuhudhuria kwao hawatakuwa wamevunja sheria.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 22 Machi baada ya kuahirishwa mara kadhaa na tayari CHADEMA wameshaandika barua kwa Mkurugenzi wa Jiji ya kuthibitisha kuwa hawajakubaliana na maamuzi hayo na wao wataenda na wanachama wao kuhudhuria.

0 comments:

Post a Comment