Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla Leo afanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kikusya kupitia Ipinda kwenda Matema kwa kiwango cha lami urefu wa Kilomita 36.7.wenye thamani ya Shilingi Bilioni 56.9 wa Fedha za ndani, pia amewaambia wananchi watalipwa fidia kulingana na tathmini inayoendelea kufanyika palipopita mradi huo amewataka wananchi wa kata tatu zilizopitiwa na mradi huo kuwa na subira tathmini inafanyika na haki ya kila mmoja itapatikana kulingana na thamani
ya Mali ambapo mradi umepita.
Mbali na fidia mradi huu ambao unajengwa kuelekea vijijini utafungua milango ya fursa za uwekezaji, watalii wataongezeka, biashara ya mazao itaongezeka kwa kasi kwa fursa hii ya mradi.


0 comments:
Post a Comment