Friday, August 5, 2016



 Imeandikwa na Le Mutuz Nation

KAMPUNI ya Camel Oil imesema uuzwaji wa kiwanja namba 130 kilichoko Block A, Manzese jijini Dar es Salaam ulizingatia taratibu zote za kisheria na kwamba hakuna sehemu iliyoghushi hati za kiwanja hicho karna inavyodaiwa. Baada ya kuona utitiri wa habari za nia ya kupotosha ukweli, Camel Oil wameonelea ni vyema wakaonyesha upande wa pili wa shilingi.

Akizungumza na  mwandishi  wetuofisini  kwake  jana,  Meneja  wa Kampuni hiyo, Mahfoudh Ally, alisema kampuni  yake  ilifata  taratibu zote za kiubinadamu na kisheria katika kuuza kiwanja hicho baada ya mmiliki wa awali, Mzee Mohamed Fakhi kushindwa kulipa deni  la  Sh bilioni 1.4. Huu ulikuwa uamuzi wa mwisho kabisa baada ya jitihada za muda mrefu, na za msingi zilizogonga mwamba baada ya ahadi hewa nyingi sana  kutoka  kwa  mdeniwa,  Mzee Mohammed.

Alisema kabla ya mwaka 2010 kampuni yake  ilifanya  biashara  kwa muda mrefu na Mzee  Mohamed  wa  Manzese  Filling  Station kuhusiana na kuuza mafuta kwa mkopo kwa makubaliano  kwamba  Camel Oil ilipwe kila mwisho wa mwezi. Camel Oil iliendelea kukipa kituo hicho mafuta lakini mmiliki wa kituo hicho aliendelea kulimbikiza deni hadi kufikia Sh bilioni 1.6 na mwaka 2012 aliacha kununua mafuta kwenye kampuni hiyo ya Camel bila kutoa taarifa yoyote, na Mzee Mohammed pamoja na mtoto wake wakatokomea  kusikofahamika.

“Tulifuatilia kujua kwanini kulikuwa na  ukimya  wa  muda  na  tulitaka kujua atalipaje deni hilo, baada ya muda kadhaa wa kumtafuta tulimpata na tukakubaliana namna ya kulipa deni hilo. Alitoa hundi ambazo baadhi zilipita na nyingi ziligonga ukuta kwani hakuwa na hela benki. Kwa mara nyingine akatokomea kusikojulikana. Jitihada za dhati


ziliendelea kumtafuta na kumsihi alipe ila palikuwa na kila dalili ya kushindwa kulipa deni. Na tulipoona anashindwa kulipa deni tuliomba kushikilia  hati mbili za viwanja  vyake  kania dhamana,” alisema.
Alisema Mzee Mohamed alikubali mwenyewe kwa maandishi kwamba viwanja vyake vishikiliwe na Camel Oil karna dhamana ya deni hilo analodaiwa, na ushahidi wote wa maandishi  upo.
Kwa masikitiko Makubwa, Camel walibaini baadaye kuwa hata viwanja wanavyotaka kuchukua karna dhamana, Mzee Mohamed alishaviweka dhamana kwenye kampuni zingine ambazo zinamdai madeni mbalimbali.
Alisema hati moja ya Viwanja cha kitalu A, kilichopo Manzese ilikuwa inashikiliwa na Kampuni ya TOTAL iliyokuwa ikimdai Mzee Mohamed Sh. 165,000,000 lakini Camel Oil ilikubali kulipa deni hilo ili kushikilia hati hiyo kwa makubaliano na Mzee Mohamed kwamba fedha hizo ziongezwe kwenye deni la awali la Sh. Bilioni 1.6, ambazo Camel Oil inamdai. Pia ushahidi wa maandishi upo.
Mahfoudh alisema kwenye mkataba wa kukubali deni iliyosainiwa Septemba mwaka 2010, Mzee Mohamed alikiri kudaiwa na Camel Oil Sh bilioni 1.6 ambazo alikubali kuzilipa kwa mujibu wa masharti na makubaliano kwenye mkataba huo, kitu ambacho hakuonyesha dalili ya kutekeleza alichokiahidi.
Mahfoudh alisema kwenye makubaliano ya mkataba huo, Mohamed ambaye ni mdaiwa alikubali kuweka dhamana kiwanja namba 130 Kitalu A Manzese chenye thamani ya Sh milioni 850 na kiwanja namba 861 na namba 862 cha Msasani Beach vyenye thamani ya Sh. 300,000,000.


Katika hatua isiyo ya kawaida na ya ajabu, ya kusikitisha na kudhalilisha, hasa kwa mtu mzima na mwenye hulka kania Mzee Mohammed, ni kwenda kula kiapo Polisi pamoja na Ardhi kwamba alipoteza hati za viwanja vyake akiwa na nia mbaya ya kudhulumu, kufisadi na kuidanganya Serikali mchana kweupe. Hiki kilikuwa kitendo kibaya na cha kitapeli. Nyaraka zote za ushahidi pia zinaonyesha kila kitu kinagaubaga.

Kweli ukistaajabu ya Musa, uatayaona ya Firauni. Baada ya utitiri wa ushahidi mweupe kabisa bila chenga, imeshangaza sana kuona mzee Mohammed anajiamini na kuzungumza habari zisizo sahihi. Karna vile hii haitoshi, baada ya kugundulika njama zake za kifisadi, Mzee Mohammed alifungua kesi ya kughushi, dhidi ya Camel Oil. Baada ya muda sio mrefu, katika muendelezo wa sinema zake, Mzee Mohammed alikiri mwenyewe kufuta kesi ya kughushi na akamuandikia barua IGP na DPP na Camel wakapata nakata. Katika barua yake, anasema aliamua kufuta kesi ya kughushi, bila ya kushurutiswa na yeyote, ila pengine nafsi ilimsuta kusema na kufanya matendo yasiyoendana na hulka pamoja na umri wake. Watu wake wa karibu, amabao majina yanahifadhiwa, waliiambia Camel Mzee Mohammed aliamini sana uganga na uchawi kuwa kwamba ana uwezo wa kuwafanya Camel Oil kuogopa au kusahau hilo deni. Pia hili lilijidhihirisha katika mikutano iliyofata, Mzee Mohammed kwa kinywa chake aliwatishia wadeni kuwa atajibadilisha kuwa NYOKA. Wadeni wakamkumbusha kisa cha Nabii Musa katika Quran tukufu, kuwa uwezo huo ni wa Allah (SW) na hata kania Allah ataamua kumbadili awe SIMBA, Wadeni hawatachoka kudai haki yao na wana imani kubwa sana Allah atajaalia haki ipatikane.



Mahfoudh alisema baada ya jitihada zote kufanyika ili Mzee Mohamed alipe deni hilo ilishindikana na ndipo walipomtafuta dalali kwa ajili  ya kuuza kiwanja cha Manzese kujaribu kufidia deni ambalo wanamdai.

Alisema Kampuni ya Udalali ya Bilo Star Debt Collectors ilipewa kazi hiyo na tarehe 3 Julai ilitoa tangazo kwenye gazeti la Mzalendo kwa ajili ya kuuza kiwanja cha Mzee Mohamed kilichoko Manzese  kama sehemu ya kufidia deni analodiwa. Ufupi, taratibu zote za msingi na kisheria  zikawa zimezingatiwa.

“Ingawa tulijua hata tukiuza kiwanja kile hatutapata kiasi tunachomdai ambacho kwa mwaka 2016 kilishapungua na deni mpaka July 2016 lilikuwa Sh. Bilioni 1.4 lakini tuliamua tu tuuze angalau tupate kitakachopatikana kuliko kukosa kabisa maana mdaiwa alionyesha dalili zote za kushindwa kulipa deni hilo na alifurukuta katika sinema na mbinu zisizo za kistaarabu,” alisema

Aidha, alisema mnada wa hadhara ulifanyika tarehe 9 Julai 2016 na Kampuni ya State Oil ndiyo ilipata kiwanja hicho kwa kununua kwa Sh bilioni moja (1,000,000,000) hivyo kuwa mmiliki halali wa kiwanja hicho namba 130, Block A Manzese jijini Dar es Salaam.

Alisema Camel Oil ilifuata hatua zote za kisheria mpaka kuuza kiwanja hicho na Mzee Mohamed baada ya kuona ameshindwa kulipa deni aliamua kuanzisha propaganda za kuichafua kampuni hiyo ili ionekane kwamba imemuonea.

“Habari anazoeneza kwamba amevamiwa kwenye kiwanja chake sio sahihi na hata nafsi yake yeye mwenyewe inajua kwamba anaeneza propaganda zisizo sahihi kutaka huruma kutoka kwa jamii maana karna nyaraka zote za kudaiwa kiasi hicho tunazo na amesaini mwenyewe, sisi



Tulichukua hati kama dhamana baada ya yeye mwenyewe kukubali sasa hatujui kwa nini Mzee mzima anahangaika” alisema

Alipofutwa na mwandishi wetu kuzungumzia mgogoro huo, Mzee Mohamed alisema suala hilo ameshalifikisha kwenye vyombo vya dola na anatarajia ukweli utajulikana hivi karibuni. Baada ya kupitia nyaraka zoote za ushindi , mwandishi alishangazwa sana na hizi propaganda zinazoenezwa bila hofu walawoga kwa Mungu . Hali kadhalika, ajabu ni kusema Mzee Mohamed hana tena imani na Police na Mahakama , baada ya kutumia njia mbalimbali anazozifahamu yeye mwenyewe, katika kupindisha ukweli, ila Mungu si Athumani, njia hizo zote zikaishia ukingoni. Sasa lawama wanatupiwa Police na Mahakama badala ya kujipanga kulipa amana za watu.

Le Mutuz Nation

0 comments:

Post a Comment