Wednesday, February 8, 2017


Mwanamitindo nguli nchini Tanzania Asia Idarus Khamsin amewataka wadau na wapenzi wa mitindo nchini kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Mwanamke ndani ya nguo nyekundu yaani Lady in Red ili waweze kununua kazi za sanaa zilizotengenezwa na wanamitindo na wasanii ambao hapo awali walikuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akizungumza na blogu ya wananchi, Asia amesema siku ya tamasha la Lady in Red siku ya Jumamosi Ravia amesema mapato yatakayopatikana katika tamasha hilo yatatumika pia katika kuvisaidia vituo viwili vinavyohusika na utoaji tiba kwa vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya.
Katika hatua nyingine Asia amesema wabunifu pamoja na wanamitindo chipukizi ndio watakaopewa nafasi kubwa katika tamasha hilo, huku akisisitiza uwepo wa ubunifu wa hali ya juu.

Kwa upande wa wakala wa mitindo James Marunda amesisitiza kwamba waandaaji wa Lady in Red wamejitahidi kuhakikisha kwamba maadili ya Mtanzania yanalindwa kwa kuhakikisha heshima ya mtanzania inalindwa.

Jemes amesema mavazi yatakayovaliwa na wanamitindo yatazingatia maadili ya kitanzania kwa ujumla.

tamasha la LADY IN RED litafanyika katika ukumbi wa KING SOLOMON HALL jumamosi FEB 11.

0 comments:

Post a Comment