Monday, February 13, 2017



Chama cha mchezo wa tenis nchini TTA kimefanikiwa kupata uongozi mpya ikiwa ni sehemu ya kutii agizo la Baraza la Michezo la Taifa nchini BMT.


Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika wanja wa Taifa jijini dar es Salaam, Denis Makoi ndie aliyefanikiwa kutwaa nafasi ya Uraisi mara baada ya kupata kura 16.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya rais wa TTA, Denis Makoi ameeleza vipaumbele vyake katika kuhakikisha mchezo wa tennis unasonga mbele.
Makoi amesema atahakikisha inapatikana michezo mbalimbali ili kuhakikisha anauinua mchezo huo hapa nchini.
Dennis Makoi- Rais TTA


Nafasi ya makamo wa Rais imekwenda kwa John Bura. Na wajumbe ni Rehema Mbegu, Riziki Salum, Mosses Mabula, na Sanjay Choksi.

0 comments:

Post a Comment