Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram na umemfollow mwanadada Wema Sepetu naamini utakuwa umeshakutana na kasumba ya kutoacha comment katika baadhi ya posts ambazo mrembo huyo anazitupia kwenye page yake.
Na hiyo ni kutokana na mrembo huyo kuanzisha mtindo wa kuwa anafunga comments katika baadhi ya posts ambazo anazitupia kwenye page yake na kuwanyima uhuru watu ambao wamemfollow kuandika chochote kwenye kile ambacho anapost.
Wapo ambao hapo mwanzo waliamini kwamba Wema anafanya hivyo kutokana na matusi ambayo huwa anakutana nayo kutoka kwa baadhi ya watu na vitu kama hivyo, ila ukweli nimekuletea hapa leo.
Perfect255 imepiga story na Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu na ametusanua mchongo mzima kuhusiana na kitendo hicho cha Wema Sepetu kuwa anafunga uwanja wa comments siku za karibuni.
“Unapoacha watu wa interact maana yake wanakupa nafasi ya kuweza kuwajibu na kufanya vitu vingine wakati application ya Wema tayari inawapa nafasi watu kumuuliza maswali na kuweza kuwajibu. Kwahiyo tunazima kwasababu huku ni free, una buy bundle yako, unapiga picha unapost halafu watu wanakuja kucomment, kwanini wasije kwenye app na wachangie angalau Tsh efu 2 tu na waweze kupata yote hayo wanayoyataka.” Alisema Martin Kadinda.
Kwa maana hiyo, Wema Sepetu huwa anazima comments ili kuwafanya watu wakalipie kwenye application yake na kuweza kufanya yote ambayo wanataka.
0 comments:
Post a Comment