Monday, February 13, 2017


Chama cha mchezo wa tennis nchini Marekani kimelazimika kwaomba radhi wachezaji wa mchezo huo kutoka Ujerumani mara baada ya chama hicho kupiga wimbo wa zamani wa Ujerumani.


Wimbo uliopigwa wakati wa michuano hiyo ulijumuisha maneno Ujermani, Ujermani katika ubeti wa kwanza, hali iliyowapelekea mashabiki wa Ujerumani pamoja na wachezaji kukasirika kutokana na kitendo hicho.
Katika taarifa toka USTA kwenda Ujerumani imesema tatizo hilo halitajirudia tena.


Wimbo wa taifa wa rasmi wa Ujerumani ulianza kutumika mwaka 1920 lakini baadae ulibadilika mara baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.

0 comments:

Post a Comment