Wakali wa hip hop Bongo, Rosa Ree na Chemical
Majani amesema itachukua muda mrefu mpaka apatikane mkali huyo kutokana na sababu alizozibainisha kuwa wanawake wengi wanafanya vizuri lakini wanahitaji ushindani zaidi ili waweze kumpata mmoja ambaye ni mkali katika nyanja zote za kuchana, mashairi mazito yenye tija kwa jamii kama ilivyokuwa kwa Fareed Kubanda, Fid Q ambaye hana mshindani kwenye muziki wa hip hop mpaka sasa.
“Kwa sasa ni mapema sana kumtafuta mkali wa 'hip hop' kwa wanawake hapa bongo maana, ukicheki kama Rosa Ree ana style tofauti na ladha ya kivyake, Chemical anandika vizuri stori japo wote ni wakali na wanafanya kitu kizuri nadhani tuwape muda wapate ushindani ili apatikane mkali”. Alisema Majani
Kwa upande mwingine Majani amesema muziki unahitaji akili nyingi ili uweze kutengeneza kazi nzuri na yenye ubunifu wa hali ya juu hivyo amewataka wasanii pamoja na 'producer' kurudi shule ili waongeze maarifa zaidi katika kazi zao.
0 comments:
Post a Comment