Mwanamitindo
Hamisa Mobetto kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiwapa mashabiki wake
sababu za kumuongelea na hii ameendelea kuifanya baada ya karibuni
kuchapisha picha zake zinazoonyesha kuwa ni mjamzito, na sasa swali
limebaki ujauzito huo ni wa nani?
Taarifa
ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa ujauzito huo ni wa Majey ambaye
ndiye baba wa mtoto wake wa kwanza na kwamba sasa wanategemea mtoto wa
pili.
Lakini
mbali na hao wanaodai kuwa ni mtoto wa Majey, wengine wanadai kuwa ni
mtoto wa Diamond Platnumz licha ya kuwa mwanamuziki huyo amekanusha kuwa
ujauzito huo si wa kwake, huku akimtaka Mobeto aseme ni ujauzito wa
nani.
Kila mmoja amekuwa akisema lake, lakini anayejua ukweli kuhusu ujauzito huo, ni Hamisa Mobeto.

0 comments:
Post a Comment