Katika maamuzi ya Mahakama yaliyotolewa Nchini Kenya Majaji wanne walisema kwamba uchaguzi haukuwa wa haki na huru hivyo ndo maana wametaka uchaguzi huo urudiwe.
Hata hivyo baada ya kufanya tamko hilo waliamua kwenda kukaa kwenye hotel ya Upper Hills iliyopo Jijini Nairobi na kuchagua chumba cha siri na kujificha pamoja na kuzima simu zao.
Pamoja na majaji hao kujificha katika hotel hiyo kwa siri bado Maafisa usalama wa kenya waliwafwata huku nia kubwa ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyata akitaka wabadilishe mawazo yao na kusema uchaguzi ulikuwa wa uhuru na haki.
Chief Judge Maraga alitangaza kuwa uchaguzi sio wa haki nakutaka uchaguzi urudiwe ambapo Maafisa usalama hao walitaka kumpa rushwa na kumtaka afute kauli hiyo na kuutanagazia uma kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki ambapo habari hizo zikavuja kwa Waandishi wa habari.
Chama cha Jubilee kilitaka Majaji angalau jaji mmoja ajitokeze aseme matokea yalikuwa ya haki na chama hicho kilishinda na walitaka jaji mmoja aseme tamko lilitolewa na Majaji wengine wanne sio sahihii.
Lakini hata hivyo mmoja wa wale majaji alisema Mambo hayawezi kuwa sawa na hawawezi kubadili maamuzi hayo na waliamua maamuzi hayo kwamba Rais Uhuru hapaswi kutangazwa rasmi kuwa rais wa kuchaguliwa na tamko la IEBC ni batili na halipo.

0 comments:
Post a Comment